“TUMECHOKA KUUAWA” WANAWAKE WASEMA.- WOMEN ON STREETS MATCHING AGAINST FEMICIDE
Written by Dayo radio on January 29, 2024
Wanawake kutoka sehemu mbalimbali humu nchini hii leo wamejitokeza na kuandamana barabarani na kupinga vikali ongezeko la mauwaji ya wanawake.
Hapa Mombasa maandamano hayo yamehusisha mashirika mbalimbali yakiwemo yale ya kutetea haki za kibinadamu ambayo yamekemea vikali uuwaji wa kiholela wa wanawake ambao umeonekana kukithiri humu nchini.
“Sisi kama wama tunapinga mauwaji ya kinyama ya wanawake yanayoendelezwa humu nchini hata sisi pia tuko na haki ya kuishi na kufanya kama vile wengine wanafanya tunaomba hili swala likomeshwe mara moja”
Wakiongozwa na Grace Oloo kutoka shirika la UJAMAA CENTRE ametaja niwakati sasa wamama waungane na kukomesha visa hivyo kwani vinawaregesha nyuma hao kama kina mama.
Ni kauli iliyoungwa mko na mkurugenzi mkuu wa shirika la LEND A VOICE AFRICA Maureen Magak na kuitaka jamii pamoja na viongozi kushikana na kupinga swala hilo badala ya kupiga siasa kila kukicha.
“Tunaomba wakenya wajitokeze ili kukataa ukatili unaondelea hapa nchini vizazi vyetu vinaangazwa kihohelela sisi kama wamama leo tunakemea mauwaji hayo na viongozi wote lazma waungane ili kukomesha huu ukatili.”
Ikumbukwe kwamba kisa cha mauwaji ya Rita Waeni ni muongoni mwa visa vilivyowahi kutokea hivi majuzi
reported by Harrison Kazungu